Words Ni Word : Sheng Poem

 

 

Usidanganywe na hii kihara
Akili ni nywele na zangu ni in-built
Unadhani poetry ni ya watu wamekosa kazi?
Hata ofisi ni word

Streets za Nairobi zimeficha siri zetu
Juu huko ndo si hujiachilia

Kama hii ni ugonjwa basi nitadedi na upele
Juu hii word imepita skin deep kwa bloodstream hadi skele
Plasma bado ni maji

Napenda kudive kwa wells za imagination
Future yangu naiona kwa mikono
Kila line naandika inanipa picha ya tomorrow

Njia ya mwoga ni fupi
Dunia imejaa madwarf
Watu wako too short kukubali ukweli
Too shocked heri waone reality kwa telly
Giza huwa na mwangaza
Ukiitembelea ka umefungua macho za akili

Unataka kukuwa successful?
Wacha nikupee siri
Uma vako na ukae hard
Masofty hawananga chao
Na usitupe mbachao kwa msala upitao
Usiwai dharau mtu
Kila hustler akona kwao

Hizi words ni panga
Zinakata hadi upepo
Na hii poetry ndo mi hushibanga

Hata nikidedi
Bado hizi mashairi zitaspeak to the living dead

Bible ya red hainanga miujiza mob za Yesu kushinda ile ya black
Zote sawa

Hakuna siku nyoka itawai zaa chura
Fimbo ya mbali haiui panya

Na mtaka cha mvunguni lazima akuwe rada

Hii word ni sick inapea conscience yangu fever
Nikona kichwa ka mayai juu ndani york imeiva…

Post Author: Eric Onyango Otieno

0 thoughts on “Words Ni Word : Sheng Poem

  • Pius khisa

    (February 5, 2014 - 1:40 pm)

    Wow, dogo hii ni kali! Hongera.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *